Monday, November 28, 2016

JOSE MOURINHO HUENDA AKAADHIBIWA NA CHAMA CHA SOKA CHA WINGEREZA

JOSE MOURINHO
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anakabiliwa na uwezekano wa kuadhibiwa tena.
Jose Mourinho alitumikia marufuku ya mechi moja dhidi ya Swansea chini ya mwezi mmoja uliopita
Hii ilikuwa ni mara ya pili kwake kufukuzwa uwanjani na mwamuzi katika kipindi cha mwezi mmoja.
Mreno huyo alifukuzwa na mwamuzi Jon Moss baada yake kuonekana kukerwa na uamuzi wa refa huyo wa kumuonesha Paul Pogba kadi ya manjano kwa kujiangusha uwanjani mechi ya dhidi ya West Ham, na akapiga chupa teke kwa hasira.
Mechi hiyo ilimalizika sare 1-1.

No comments:

Post a Comment