Wednesday, November 30, 2016

NIKE WATOA VIATU VIPYA

Air Max CB34
Kampuni ya vifaa vya michezo na mavazi Nike wametoa bidhaa mpya ni kiatu ambacho huchezewa basketball na mitoko ya hapa na pale Air Max CB34 kwa jina jingine wanakiita “Triple White” kupitia kwa wahusika wakampuni wanasema wameamua kukitoa bila kuwaambia wateja kimya kimya kwa kujua bidhaa yao ni bora,wanasema kiatu chao ni imara na chenye soli isiyoweza kukatika na kamba ambazo hufungwa kirahisi na kumfanya mteja kukipendeza zaidi.
Air Max CB34
Air Max CB34

Aiza viatu hivi vitatoka vikiwa na rangi mbalimbali kulinga na mahitaji ya mteja na vitakuwepo kote kwenye maduka ya Nike na mawakala wao ili kuwafikia wateja.

VIDEO MPYA YA FETTY WAP (MAKE YOU FEEL GOOD)

Rapper wa muziki wa Marekani Fetty Wap mkali wa single Trap queen ilifanya vizuri kote duniani.leo kaja na kitu kingine Make you feel Good ni ngoma inayotoka kwenye mixtape yake mpya inayoitwa Zoovier .unaweza kucheki video hapa https://youtu.be/eRsSxEVmSnw

DONALD TRUMP KUTANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI

Donald Trump
Rais mteule wa Marekani Donald Trump anajiandaa kutangaza mawaziri zaidi watakaohudumia utawala wake.
Ripoti zinasema kwamba Trump atamteua mshirika wake wa kibiashara wa zamani Steven Mnuchin kama waziri wa fedha.
Wawili hao walikuwa wanamiliki Goldman Sachs, kampuni ambayo Trump aliikashifu wakati wa kampeni zake.
Pia ameshiriki mazungumzo na Mitt Romney, ambaye anakisiwa kuwa mwaniaji wa wadhfa wa waziri wa mambo ya kigeni.

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA KWENYE GEREZA LA UKONGA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar -Es - Salaam na kupiga marufuku uuzwaji wa sare za majeshi nchini humo na watu binafsi na kutaka wale wote wanaouza sare hizo wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja.

 Rais Magufuli amepiga marufuku hiyo kufuatia maelezo kutoka kwa baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza kuwa wamekuwa wakinunua sare za jeshi hilo kutoka kwa watu binafsi kinyume na taratibu za majeshi na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua mara moja wale wote watakaobainika kuuza sare za majeshi.

Hali kadhalika Rais magufuli amepiga marufuku kwa majeshi yote nchini mwake kuingia ubia na watu binafsi kupangisha ama kuuza maeneo yao kwa ajili ya kufanya biashara na kutaka maeneo yote ya majeshi yabaki katika jeshi husika.''Haiwezekani sare za majeshi yetu hapa nchini kuuzwa na watu binafsi hilo haliwezekani kamwe labda baada ya kumaliza muda wangu , amesema Rais magufuli''

 Aidha Rais Magufuli ametoa shilingi Bilioni Kumi kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kujenga nyumba mpya zitakazotumika kwa ajili ya makazi ya askari wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Ukonga jijini DSM.

 Hatua hiyo inafuatia kilio cha askari Magereza kuwa wengi wao wamekuwa wakiishi uaraiani kitu ambacho ni tofauti na taratibu za majeshi na hata kuzorotesha utendaji kazi wa askari wa Jeshi hilo.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli pia ameagiza Jeshi la Magereza kuhakikisha wafungwa wanatumika katika uzalishaji mali badala ya mfumo wa sasa ambapo baadhi ya wafungwa wamekuwa wakitumia rasilimali za serikali bila kuzifanyia kazi.

 Rais Magufuli amewahakikishia Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kuwa serikali itaendelea kuboresha maslahi yao na vitendea kazi kama inavyofanya kwa majeshi mengine nchini Tanzania.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli,akiwa katika gereza la Ukonga.

Tuesday, November 29, 2016

VIDEO MPYA YA NAVY KENZO (FEEL GOOD)

Navy Kenzo wamerudi na mdundo mwingi Feel Good,video wamefanyia South Africa Directer wa video hii ni Justin Campos.unawe kuitazama video hapa https://youtu.be/xmp8CjOg8NM

Monday, November 28, 2016

VIDEO MPYA DJ MAPHORISA NA WIZ KID (GOOD LOVE)

DJ MAPHORISA NA WIZ KID
Dj maphorisa na Wiz kid walifanya ngoma awali ya Soweto baby ikafanya poa kote Africa na kuchukua Tuzo za MTV zilizofanyika South africa ila safari hii wameamua kurudi tena na upya kwa ngoma inayoitwa Good Love .producer akiwa Dj Maphorisa na Nana Rouge.Unaweza kuicheki video hapa https://youtu.be/_bhs0s0nRbs

GRACE MATATA KATOA VIDEO MPYA (UTANIFAA)

Grace Matata baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu na kufanya kazi mziki kwa kupiga kwenye band.leo ameamua kutowa zawadi kwa mashabiki zake wimbo unaitwa Unanifaa alomshirikisha Emmagripa,unaweza kuitazama video hapah https://youtu.be/cO-YHzMFlc0

JOSE MOURINHO HUENDA AKAADHIBIWA NA CHAMA CHA SOKA CHA WINGEREZA

JOSE MOURINHO
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anakabiliwa na uwezekano wa kuadhibiwa tena.
Jose Mourinho alitumikia marufuku ya mechi moja dhidi ya Swansea chini ya mwezi mmoja uliopita
Hii ilikuwa ni mara ya pili kwake kufukuzwa uwanjani na mwamuzi katika kipindi cha mwezi mmoja.
Mreno huyo alifukuzwa na mwamuzi Jon Moss baada yake kuonekana kukerwa na uamuzi wa refa huyo wa kumuonesha Paul Pogba kadi ya manjano kwa kujiangusha uwanjani mechi ya dhidi ya West Ham, na akapiga chupa teke kwa hasira.
Mechi hiyo ilimalizika sare 1-1.

WIZARA YA ELIMU JANA IMETOA TAMKO RASIMI KUPTIA KWA WAZIRI WA ELIM JOYCE NDALICHAKO

Profesa Joyce Ndalichako
Mara hii, ikiwa yaliyomo katika Hotuba yake yatatekelezwa, utakuwa mwisho wa moja ya mifumo iliyokuwepo ambapo mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne angeweza kuamua kusoma ngazi ya Diploma yaani Stashahada badala ya kupitia katika ngazi ya kidato cha sita.
Waziri huyo wa Elimu anaongeza kuwa wanafunzi wasiofaulu katika kidato cha nne wamekuwa wakienda kusoma ngazi ya cheti, kisha Stashahada na baadaye wakipenya na kuelekea katika Shahada yaani digrii lakini sasa watalazimika kupitia katika ngazi ya kidato cha sita.
Ambao hawatapitia katika safari ya kidato cha sita ni wale watakaofaulu katika kidato cha nne na kuchaguliwa kwenda kusoma katika vyuo vya ufundi daraja la kati.
Mfumo mwingine pia utakaaoathirika ni ule ambao mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita lakini akashindwa kukamilisha vigezo kadhaa vinavyotakiwa katika vyuo vikuu alikuwa anapata nafasi ya kufanya masomo ya muda yaani 'Foundation Course' katika Chuo kikuu huria cha Tanzania na kama angefaulu angeruhusiwa kuendelea na masomo ngazi ya degree.

Sunday, November 27, 2016

CUBA INAADHIMISHA SIKU TISA ZA MAOMBOLEZO KUFATIA KUFARIKI KWA FIDEL CASTRO

Fidel Castro
Serekali ya Cuba imetangaza siku tisa za maombolezo ya kifo cha rais mstaafu wa nchi hiyo Fidel Castro,huku ukiwekwa wazi utaratibu wa mazishi yake kwa kufuata usiya wake mwenye marehem ,Mwili wake, utachomwa hadi kuwa majivu kama alivyotaka, katika sherehe ya kibinafsi, ambapo majivu yake yatazungushwa katika msafara maalumu kote nchini kabla ya kuzikwa katika Makaburi ya Mji wa Santiago Desemba tarehe nne.

Akiwa kiongozi mwenye mrengo wa kushoto na mwanamapinduzi msifiwa, alipendwa na kuchukiwa na watu mbalimbali kote duniani
Fidel Castro

ADIDAS KUTENGENEZA JEZI ZA PLASTIKI ZA REAL MADRID

Kwa wale wapenzi wa soka huenda hii habari wameshaisikia kampuni ya vifaa vya michezo duniani Adida inayofanya kazi ya kutengeneza jezi za Real madrid imeamua kuwatengenezea jezi za plastiki timu hiyo na tiyari zimesha valiwa na time.Adidas wao wanasema jezi hizo zimetengenezwa kwa matiliyo ya plastiki za makopo ya machupa ya maji,makopo 28 hutumika kutengenezea jezi moja

Saturday, November 26, 2016

FIDEL CASTRO AFARIKI DUNIA

Fidel Castro
"Amiri Jeshi mkuu wa mapinduzi ya Cuba alifariki dunia mwendo wa saa 22:29 usiku huu (03:29 GMT Jumamosi)," Rais Raul Castro ametangaza.Fidel Castro alitawala Cuba kama taifa la chama kimoja kwa karibu miaka 50 kabla ya kakake Raul kuchukua nchi 2008

Wasifu wa Fidel Castro Kiongozi huyo mwenye utata alisifiwa na wafuasi wake kama kiongozi wa ujamaa, askari mwanasiasa ambaye aliirejesha Cuba mikononi mwa watu. Lakini alikabiliwa na shutuma kwa kuwazima wapinzani wake kwa njia ya mateso na kwa kuwa na sera ambazo ziliporomosha uchumi wa Cuba. Fidel Alejandro Castro Ruz alizaliwa tarehe 13 Agosti 1926, nje ya ndoa ya familia ya mkulima bwanyenye , Angel María Bautista Castro y Argiz, ammbaye alihamia Cuba kutoka Uhispania.
Mama yake , Lina Ruz González alikuwa kijakazi aliyefanya shughuli za shamba ambaye baadae alikuwa mpenzi wa baba yake ,na baadae ,baada ya kuzaliwa kwa Fidel, akawa mkewe.
Fidel Castro
Papa John Paul II akisalimiana na Fidel Castro
Castro (Kushoto) akiwa na Che Guevara wakati wa vita vya msituni
Castro alisoma katika shule ya kikatoliki mjini Santiago kabla ya kujiunga na chuo kinachoendeshwa na makasisi wa Jesuit- kilicho El Colegio de Belen jijini Havana.
Hata hivyo, alishindwa kimasomo , na badala yake alipendelea kutumia muda wake mwingi katika shughuli za michezo.
Ilikuwa wakati anasomea sheria katika Chuo Kikuu cha Havana kati kati ya miaka ya -1940s ndipo alipokuwa mwanaharakati wa siasa, na kuimarisha ujuzi wake wa kuzungumza hadharani.
Malengo yake yalikuwa ni pamoja serikali ya Cuba, iliyoongozwa na Ramon Grau, ambayo ilikumbwa na shutuma za ufisadi wakati huo.
Ghasia za maandamano ya upinzani ziligeuka kuwa maisha ya kila siku na Castro akajipata akilengwa na polisi.
Pia alikuwa miongoni mwa watu waliopanga njama za mapinduzi ya kumg'oa mamlakani Rafael Trujillo, kiongozi wa mrengo wa kulia wa Dominican Republic , lakini jaribio hilo lilishindwa baada ya na Marekani kuingilia kati.
Mnamo mwaka 1948 Castro alimuoa Mirta Diaz-Balart, mwanae mwanasiasa tajiri nchini Cuba. Mbali na kumtia msukumo wa kujiunga na wasomi wa nchi, aligeuka kuwa na itikadi za he Kimaxist
Aliamini matatizo ya Cuba ya kiuchumi yalikuwa ni matokeo ya ubepari usioweza kudhibitiwa ambao unaweza kutatuliwa tu kwa mapinduzi.
Baada ya kuhitimu masomo Castro alizindua shughuli za kisheria lakini zilishindwa kufanikiwa na aliendelea kuingia katika mzozo wa madeni.
Alisalia kuwa mwanaharakati wa kisiasa, akishiriki katika misururu ya maandamano ya mara kwa mara ya ghasia.
Mnamo mwaka 1952 Fulgencio Batista alifanya mapinduzi ya kijeshi yaliyomg'oa madarakani rais wa Cuba , Carlos Prío.
Sera ya Batista ya uhusiano wa karibu na Marekani na kukandamiza mashirika ya kijamaa vilikuwa pingamizi kwa kwa imani za kimsingi za siasa za Castro.
Baada ya kushindwa kisheria, Castro alibuni shirika lililoitwa The Movement, lililoendesha shughuli zake kisiri kwa lengo la kuung'oa madarakani utawala wa Batista.
Cuba palikuwa mahala pa watu matajiri kujivinjari, na nchi iliongozwa na kiasi kikubwa na magenge ya wahalifu . Ukahaba ,wacheza kamali na walanguzi wa mihadarati vilikithiri.
Mwezi Julai 1953 Castro alipanga shambulio dhidi ya kituo cha kijeshi cha Moncada akaribu na Santiago ili kupora silahga kwa ajili ya kuzitumia katika harakati za kivita.
Shambulio lilishindwa na wanamageuzi waliuawa ama kukamatwa . Castro alikuwa mmoja wa wafungwa kadhaa waliofikishwa mahakamani mnamo mwezi Septemba 1953.
Castro alitumia muonekano wake mahakamani kutangaza maasi yaliyotekelezwa na jeshi jambo ambalo baadae lilimpatia umaarufu, hususan miongoni mwa waandishi wa habari wa kigeni ambao waliruhusiwa kuhudhuria kesi hiyo.
Guerrilla warfare
Alihukumia kifungo cha miaka 15 jela . Baadae aliachiliwa hru kufuatia tangazo la huruma la jumla mnamo mwezi Mei 1955 baada ya kutumikia kifungo hicho kwa miezi 19 pekeekatika mazingira bora kiasi.
Katika kipindi hiki kifupi gerezani alimtaliki mkewe na kujiimarisha zaidi katika sera za kimaxist.
Kutokana na Batista kuendela kuwakamata wapinzani wake , Castro alitorokea Mexico kuepuka kutuwa nguvuni . Huko alikutana na mwana mageuzi kijana aliyeitwa Ernesto "Che" Guevara.
Mnamo mwezi Novemba 1956, Castro alirejea Cuba akiambatana na wanajeshi 81 akwenye ndege iliyokuwa na uwezo wa kuwabeba watu 12 pekee.
Makao makuu ya chama yalitafuta hifadhi katika milima ya Sierra Maestra . Kutoka kwenye ngome hii Castro alizingua vita vya msituni dhidi ya utawala wa Havana.
Tarehe 2 Januari, 1959, jeshi la waasi likaingia katika mji mkuu wa Cubanna Batista akatoroka.
Mamia ya wafuasi wa zamani wa Batista walinyongwa baada ya kesi ambazo wageni wengi waliziona kuwa hazikuwa za haki.
Castro ralijibu kwa kusisitiza kwamba " Haki ya mageuzi haina misingi ya kisheria ya kubadili tabia ama mawazo , bali inazingatia uwajibikaji wa maadili ".
Serikali mpya ya Cuba iliahidi kurejesha ardhi kwa watu na kulinda haki za maskini.
Lakini mara moja serikali ilianza kulazimisha mfumo wa chama kimoja cha kisiasa . Mamia ya watu walitupwa jela na kwenye kambi za kutumikisha kazi za sulba kama wafungwa wa kisiasa.
Maelfu ya waCuba hususan wenye kipato cha kadri wakalazimika kuikimbia nchi yao

Castro alisisitiza kwamba fikra zake zilikuwa ni bora zinajali kwanza maslahi ya watu wa Cuba.
"hakuna ujamaa au umaxist , bali uwakilishi wa demokrasia na haki ya kijamiikatika mpango bora wa uchumi ," alisema wakati huo.
Mnamo 1960, Fidel Castro naliwapatia uraia wamarekani woote waliokuwa wanamiliki biashara katika kisiwa hicho.
Kujibu hatua hiyo, utawala wa Washington ulimuwekea vikwazo vya kibiashara vilivyo tarajiwa kudumu kwa karne ya 21st century.
Castro alidai kuwa alilazimishwa kuingia katika mikono ya muungao wa Usovieti na kiongozi wake , Nikita Khrushchev, ingawa baadhi ya wachanganuzi walisema aliingia katika muungano huo USSR kwa utashi wake mwenyewe.
Iwe sababu yoyote ile, taifa la Cuba liligeuka kuwa uwanja wa mapamabano ya vita baridi vya dunia.
Mwezi Aprili 1961, Marekani ilijaribu kuipindua serikali ya Castro kwa kuwapatia mafunzo wanajeshi binafsi wa Cuba waliokuwa ukimbizini ili kuvamia kisiwa hicho.
Katika mwambao wa Pigs,vikosi vya Cuba vilikabili majeshi ya uvamizi , na kuwauwa wengi huku 1,000 wakikamatwa. Fidel Castro alikuwa ameonja malaka kwa njia ya damu kwa hivyo asingeweza kuwasamehe.
Mwaka mmoja baadae, ndege za uchunguzi za Marekani ziligundua makombora ya Usovieti wakati zilipokuwa njiani kuelekea maeneo ya Cuba.
Dunia ilishtushwa na uwezekano wa kutokea vita vya nuklia .
"msururu wa maeneo yenye makombora ya masafa marefu ya kivita sasa yanaandaliwa katika kisiwa kilichofungwa. Lengo la ngome hizi za makombora haliwezi kuwa lingine zaidi ya kutoa uwezo wa kufanya mashambulio ya nuklia dhidi ya mataifa ya magharibi ," alionya rais John F Kennedy.
Mataifa yenye nguvu duniani yalibaki kushuhudia kinachoendelea lakini ni rais Khrushchev pekee ambaye aliweza kuchukua hatua kwanza na kuondoa makombora yake nje ya Cuba baada Marekani kukubali kuondoa kisiri silaha zake kutoka Uturuki.
Fidel Castro, hata hivyo , alikuwa tayari ni adui wa Marekani namba moja. Maafisa wa ujasusi wa Marekani CIA walijaribu kumuua , katika kisa kilichojulikana kama -Operation Mongoose ambapo mbinu mojawapo ilikuwa apewe sigara iliyokuwa imesheheni vilipuzi.
Mbinu nyingine zilikuwa za kushangaza , ikiwemo mojawapo ya kumfanya ndevu zake zianguke ili kumfanya awe na sura ya kuto heshimika.
Muungano wa Usovieti ulimwaga pesa ndani ya Cuba. Ulinunua mavuno ya sukari inayozalishwa kisiwani humo na meli zake kurejea na zimesheheni na bidhaa nyingine, kama vile chakula kilichokua kinahitajika ili kukabiliana na vikwazo vya Marekani vya biashara.
Licha ya utegemezi wa msaada kutoka mataifa ya Usovieti , Castro aliiongoza Cuba kuwa taifa jipya lisilokuwa na mafungamano yoyote.
Hata hivyo, aliegamia hasa Afrika, ambako alituma majeshi kuunga mkono wapiganaji wa msituni waliokuwa na sera za kimaxist katika nchi za Angola na Msumbiji.
Kati kati ya miaka ya 1980 , hata hivyo, siasa za dunia za maeneo zilibadili mkondo wake . Ilikuwa ni enzi ya Mikhail Gorbachev, sera za glasnost na perestroika, na zilidhihirika wazi kuwa kinyume na mageuzi ya Castro.
Utawala wa Moscow ukakata uhusiano wa kiuchumi maramoja na Cuba kwa kukataa kata kata kununua sukari ya Cuba
Akiwa bado chini ya vikwazo vya Marekani na kukatwa wa huduma muhimu za mataifa ya Soviet , uhaba wa kudumu wa bidhaa na ukosefu wa akiba ya bidhaa vilidhihirika ndani ya Cuba
Jazba ilipanda huku misururu ya kupata ikiendelea kurefuka.
Taifa ambalo Fidel Castro aliita lililoendelea zaidi duniani, hali ya maisha ilikuwa mbaya.
Katika kati ya miaka ya -1990s, waCuba wengi walikuwa wamechoshwa na hali nchini mwao. Maelfu walianza kutoroka kupitia njia ya maji hadi Florida wakiwa na ndoto ya kuishi maisha bora zaidi. Wengi walikufa maji, lakini ilikuwa kura tosha ya kutokuwa na imani na Castro.
Hata hivyo Cuba ilirekodi baadhi ya mafanikio ya kufurahisha ndani ya nchi. Huduma bora za matibabu zilitolewa bure kwa wote , na viwango vya vifo vya watoto wachanga wa vililinganishwa na vile vya mataifa tajiri duniani.
Katika miaka iliyofuata , Castro alionekana mtulivu . Mwaka 1998 alitembelewa na Papa John Paul II, jambo ambalo halingeweza hata kufikiriwa miaka mitano ya awali.
Wakati huo Papa aliilaumu Cuba kwa ukiukaji wake wa haki za binadamu , na kumuaibisha Castro mbele ya vyombo vya habari vya dunia.
Fidel Castro alikuwa amebuni utambulisho wake kama mjamaa wa Caribbean ambao kwa miaka kumi iliyopita , alilazimika kuukumbatia , pole pole alianzisha mabadiliko machache ya biashara huria ili kulinda mageuzi yake.
Tarehe 31 Julai 2006,siku chache tu kabla ya maadhimisho ya mwaka wake wa 80 wa kuzaliwa, Castro alikabidhi mamlaka ya muda kwa Raul baada ya kufanyiwa upasuaji wa dharura wa utumbo.
Afya yake iliendelea kudhoofika. Mapema mwaka 2008, Castro alitangaza kwamba hatakubali nyadfa za urais na amiri jeshi mkuu katika mkutano kuu ujao wa kitaifa.
Katika barua iliyochapishwa katika gazeti rasmi la kijamaa, alikaririwa akisema kuwa : " Ni kudanganya nafsi yangu kuchukua majukumu yanayohitaji kutembea na kujitolea , wakati siko katika hali ya kimwili inayoniruhusu kufanya hivyo ."
Alijiondoa kwa kiasi kikubwa katika maisha ya umma , huku akiandika taarifa zilizochapishwa katika vyombo vya habari vya kitaifachini ya kichwa cha habari...Tathmini ya maisha ya amir Fidel.
Alijitokeza tena mwezi Julai 2010, alipoonekana mbele ya umma tangu augue, akiwasalimia wafanyakazi na kuhojiwa na televisheni ambapo alijadili kuhusu hali ya wasi wasi baina ya Marekani na Iran pamoja na Korea kaskazini.
Mwezi uliofuatia Castro alitoa hotuba yake ya kwanza katika bunge la taifa baada ya miaka minne, akiitaka Marekani kuacha kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran au Korea Kaskazini akionya kutokea kwa maafa ya nuklia ikiwa uhasama utazidi.
Alipoulizwa a ikiwa Castro anaweza kuingia tena katika serikali , waziri wa utamaduni Abel Prieto aliiambia BBC: "nadhani wakati wote amekuwa katika maisha ya siasa za Cuba lakini hayuko serikalini. Wakati wote amekuwa makini kwa hilo. Vita vyake vikuu ni kuhusu masuala ya kimataifa."
Tangazo la rais Obama la Disemba 2014 la mwanzo wa kumalizika kwa vikwazo vya Marekani vya biashara na vinginevyo lilionekana kama matumaini katika kile kilichokuwa uadui wa nusu karne uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Castro aliafiki hatua hiyo aliyoielezea kuwa " hatua nzuri ya kutafuta mani ya kikanda ", lakini hakuiamini serikali ya Marekani.
Wakati waCuba wengi bila shaka hawakumpenda Castro, wengine walimpenda kwa dhati . Walimuona kama David ambaye aliweza kukabiliana na Goliath wa Marekani.
Kwao Castro alikuwa Cuba na Cuba ilikuwa Castro.

MWANA FA NA VANESSA MDEE (DUME SURUALI) VIDEO UNAWEZA KUITAZAMA

Mwana Fa kaitoa video ya DUME SURUALI alomshiriki Vanessa Mdee.unaweza kuitaza hapa https://youtu.be/hmCy6ilXE4s

Wednesday, November 23, 2016

VIDEO MPYA DARASA NA BEN PAUL (MUZIKI)

Darasa katuletea nyimbo mpya safari hii MUZIKI alomshirikisha Ben Paul video imefanywa na Hascana unaweza icheki hapa  https://youtu.be/DWyiC2CBtyI

DELA NDIYE ALIYERUDIA WIMBO ADELE(HELLO) KWA LUGHA YA KISWAHILI

Dela
Dela
Adeline Maranga jina maarufu Dela jina hili linaweza likawa si geni kwako kwenye muziki hasa pale aliporudia kibao cha mkali wa mziki wa taratibu ADELE  kupitia wimbo wake wa Hello ulofanya vizuri sana duniani kote na kumuingizia mamillioni ya pesa na huku kuacha ngumzo kwa kurudiwa na mamia  ya watu kuimba kama yeye alivyo imba.kwa hapa kwetu Tanzania wimbo huo ulirudiwa na msaani Beka Ibrozama na kuimba vizuri sana na kusikilizwa na watanzania na wengine kutokujua hata uhalisi wa mwenye nyimbo.lakini kubwa lilistua afrika mashariki ni baada ya Dela kuimba kwa lugha ya kiswahili na bahati nzuri nyimbo aloimba Dela yenye maneno ya kiswahili ili weza kufanya vizuri hata nje pale ilipochezwa kwenye vituo vya radio vya wingereza na hata yeye mwenyewe Adele aliposikia alimpongeza sana Dela kwa alichokifanya .unaweza kuitazma video hiyo hapa https://youtu.be/3A_6ukgyNvQ

Tuesday, November 22, 2016

VIDEO MPYA YA RICH MAVOKO FT DIAMOND PLATNUM IMETOKA

Rich Mavoko ameachia video dakika chache zilizopita akiwa kamshirikisha Diamond platnum nyimbo yenye inatwa KOKOROKO.pruducer wa nyimbo hii ni Lizer na Abby Dady .unaweza Itazama video hapa https://youtu.be/Pouc1n__1HI

FAHAM JAMAA ANAYEINGIZA KILA SIKU DOLLA 5 KWA KUBRASH VIATU

Idris
kama mtu wa kupenda kujua ya mtandao basi utakuwa umekutana na hili la NIGERIA .Idris, raia wa Nigeria mwenye umri wa miaka 21, amekuwa akipaka viatu rangi kwa muda wa miaka mitatu na amekuwa akipata pesa zaidi ya dolla 5.watu wengi wa jiji ABUJA wamekuwa wanadharau sana kazi kwa kutokujua wanaingiza kiasi gani? ambacho kinaendesha maisha yangu ,Maneno hayo kayasema Idris
Anasema hungiza pesa kushinda hata wafanyakazi wa serikalini ,stahiri yake ni sawa hapa vijana wa kitanzania wanvyo pita kila mtaa akipaka rangi wakinadada na yeye hupita kila kona ya jiji la ABUJA kwa wateja wake kupaka rangi viatu
Idris

WIMBO MPYA MWANA FA NA VANESSA MDEE

Mwana FA karudi tena na mdundo mwingine alo shirikiana mkali mwingine Vanessa Mdee ,nyimbo imefanyika Mj record chini ya produced Daxo Chali unaweza kudownload hapa https://mkito.com/song/14331

Sunday, November 20, 2016

WATER CHILAMBO ATOA VIDEO MPYA YA GOSPEL

Water Chilambo hii ndo video yake ya kwanza baada ya kuacha mziki wa kidunia na kuamua kuimba Gospel ili kumwimbia mwenyezi Mungu ,unaweza tazama hapa  https://youtu.be/GHi3DAlMnA0

DAVIDO AMETUNDOSHEA VIDEO NYINGINE

Star wa Nigeria Davido ametudonoshea mdundo mwingine unaitwa Coolest kid in Africa alimshirikisha Nasty c Directer wa video hii ni Sesan unaweza icheki hapa  youtu.be/QGrxqOcZpZU

Tuesday, November 15, 2016

JOSEPH KABILA AMESEMA HATOWANIA MADARAKA YA URAIS TENA

 Joseph Kabila
Kumekuwa na vurugu za kisiasa katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kupiti vyama vya upizani vya nchi hiyo kwa kutaka kumwondoa Joseph Kabila kuto wania madaraka tena uchanguzi ujao.kumekuwa na maandamano kama yello card ikiashilia kumtoa madaraka Joseph Kabila.Jana waziri wa nchi hiyo amejiuzuru na kuwapa wapinza cheo hicho.

Taharifa zilizotolewa na serikali ya nchi hiyo nikuwa Joseph Kabila ameruhutubia Bunge leo na amekubali kutoa wania tena madaraka ya nchi hiyo na ameomba kuwe na amani na amekubali sababu ya kutaka amani

Joseph Kabila amesema "Kwa wale ambao wanaingilia kati maisha yangu ya siasa kila siku, nina sema asante lakini wafahamu ya kwamba Jahmuri ya Kidemorisia ya Congo ni nchi inayoongozwa na katiba hatujakiuka katiba na tutaendelea kuiheshimu. Kwa mda huu kilicho muhimu ni kuangalia maisha ya wakongomani". 

MODEL CALISAH VIDEO YAKE YA VUJA AKIWA NA WEMA

Calisah
Model wa mavazi na video Calisah amejikuta akiwa kwenye wakati mgum kwa kipindi hiki baada ya video kuvuja akiwa kimahaba na Wema wakipiga madeda.yeye mwenyewe anasema haelewi nini? kilichoteka.Anasema Wema ni mtu ambaye walikuwa kimapenzi kwa siri na alikuwa hapendi ndugu zake wajue na hiyo video walirekodi wakiwa na furaha na alikuwa anajua ni ngum kwa video hiyo kuvuja kwa kuwa wao wa wili ndo walikuwa nayo video hiyo,anasema akashanga kuona video ikilink kwenye mtandao whatsaap na alipojaribu kumuuliza Wema alisema hajui zaidi Wema naye aliishi kumlaum kwa kusambaza video hiyo.

Calisah anasema kwa ishu iliyotokea imeweza kumletea doa kwenye maisha yake kwa mikataba yake kuvunjika na makampuni alokuwa anafanya nayo kazi alitakiwa kitu kama hicho kisitoke kwake.nakubwa kwake ambalo linamweka kwenye wakati mgum kwa kufiwa na Bibi yake ambaye alipatwa na mshituko baada ya Bibi yake kuona video hiyo na kupandisha presha na kupelekea umauti.
Calisah na Wema

Monday, November 14, 2016

JACKIE CHAN AMETUNUKIWA TUZO YA HESHIMA YA OSCAR.

Jackie Chan
Kwa wale wapenzi wa filam na hata si wapanzi wa filam jina hili halitakuwa si geni kwako JACKIE CHAN kipenzi cha wachina wengi na ulimwenguni kote kwa uhodali wa kucheza filam.amezaliwa mnamo tarehe 7.4.1954 akiwa na miaka 62 huko Victoria Peak, Hong Kong 

Jana ilikuwa siku yenye furaha kwake kwa kupewa tuzo ya heshima kwa kucheza filam takribani 200,tuzo hizo zimetolewa Marekani katika jiji la Los Angeles.
Chris Tucker akimkabidhi tuzo Jackie Chan
Jackie Chan akiwa pozi la picha ya pamoja na Syveter Stallone
Jackie Chan akipongezwa na Syveter Stallone Rambo

RAPA MEEK MILL AMETOA MIXTAPE

MEEK MILL
Rapa wa Mareakani Robert Williams a.k.a MEEK MILL ametoa mixtape yake ya Nne 2016 baada ya ile ya awali kufanya vizuri ilikuwa inatwa Dreams worth more than money iliyotoka mwaka 2015 ilikuwa na hit song kibao.DC4 ndo mixtape aloiachia tarehe 28 october 2016 yenye track 14 ,imetoka kwenye Maybach Music Group and Atlantic,huku akiwa kaachia nyimbo The difference alomshirikisha rapa QUAVO aloifanyia video.mixtape hii inashika nafasi ya 3 kwenye Billbord Chat.Track zilizomo kwenye mixtape hiyo
1. “Intro”
2. “Blessed”
3.“Litty” feat. Tory Lanez
4. “Shine”
5. “Froze” feat. Lil Uzi Vert & Nicki Minaj
6. “Difference” feat. Quavo
7. “Lights Out” feat. Don Q
8. “Blue Notes”
9 . “Offended” feat. Young Thug & 21 Savage
10. “You Know” feat. YFN Lucci
11. “Way Up” feat. Tracy T
12. “2 Wrongs” feat. Guordan Banks & Pusha T
13 . “Tony Story”
DC4 MIXTAPE COVER
14. "Outro" feat. Lil Snupe & French Montana




Sunday, November 13, 2016

DONALD TRUMP AFANYA UTEUZI

Donald Trump
Rais mteule wa Marekani, DONALD TRUMP, amemteua mwenyekiti wa kamati ya taifa ya chama cha Republican, Reince Priebus, kutumika kama mkuu wa wafanyakazi.

Reince Piebus
 REINCE PIEBUS ana uhusiano wa karibu na spika wa baraza la wawakilishi Paul Ryan. Wandishi wa wa habari wanaarifu kwamba uteuzi wa Piebus unaweza kuwaudhi wafuasi wake wa hali ya chini na hii inaashiria kwamba uongozi ujao unalenga kufanya kazi kwa karibu na baraza la Congress kujihakikishia ushindi wa mapema wa baraza hilo.

AIRFORCE ONE NDO NDEGE INAYOTUMIWA NA MARAIS WA MAREKANI

AIRFORCE ONE ni ndege ya taifa la Marekani inayotumiwa na marais wake ndege hii ilikuwa inatumwa na BARACK OBAMA ,ambayo aliwahi kutua nayo Tanzania katika shughuli zake za kikazi na pia ndege hii itatumiwa na rais mteule bwana DONALD TRUMP pindi atakapo apishwa kuwa rais wa taifa hilo.Ndege hii inavyumba ambavyo vitengenezwa kisasa na ofisi ndogo ya Ikilu amabayo rais huweza kukaa na kufanya kazi zake .imefungwa mitambo maalum ambayo ni ngumu kushambuliwa