Majaribio ya chanjo cha ugonjwa wa Ebola yamebainika kuwa yana uwezo na nguvu zaidi dhidi ya virusi vya ugonjwa huo hatari.
Majaribio
yake yamefanyiwa nchini Guinea, mojawepo ya mataifa ya Afrika magharibi
ambayo yalikumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo, ambao ulimalizika mwaka
huu.Matokeo ya mwisho ya majaribio hayo, yaliyochapishwa kwenye jarida la maswala ya matibabu linalochapishwa nchini Uingereza, The Lancet, yanaonyesha kuwa takriban watu elfu sita waliopata chanjo hiyo, walionekana kuwa bila ugonjwa huyo siku kumi baadaye.
No comments:
Post a Comment