![]() |
JOSE MOURINHO |
Chama cha soka cha England Fa
kimemfungia Meneja wa Manchester United Jose Mourinho mchezo mmoja
pamoja kumtoza faini ya pauni 16,000.
Adhabu hizo zimetokana na
kosa lake la kuipiga teke chupa ya maji wakati wa mechi ya jumapili
dhidi ya West Ham alipokasirishwa na mwamuzi Jonathan Moss kumuonyesha
kadi ya njano Paul Pogba badala ya wao kupewa Frikiki.Jose hatakuwepo katika benchi la ufundi la timu yake ikicheza mechi ya robo fainali ya kombe la ligi dhidi ya West Ham uwanjani old trafford usiku huu.
Hii ni mara ya pili kwa Mourinho kupata adhabu hiyo mara ya kwa alipigwa faini pauni 50,000 baada ya kutoa kauli dhidi ya mwamuzi Anthony Taylor, kabla ya Mechi hiyo iliyochezwa Oktoba 17 dhidi ya Liverpool.
No comments:
Post a Comment